You are currently viewing WAZIRI MURKOMEN ATAMBUA MCHANGO WA KIKOSI MAALUM CHA OPARESHENI SOG KATIKA KUREJESHA UTULIVU NORTHRIFT

WAZIRI MURKOMEN ATAMBUA MCHANGO WA KIKOSI MAALUM CHA OPARESHENI SOG KATIKA KUREJESHA UTULIVU NORTHRIFT

Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen, amewapongeza maafisa wa Kikosi Maalum cha Operesheni, SOG, kufuatia  juhudi zao za kurejesha amani katika maeneo ya kaskazini mwa  bonde la ufa yaliyokabiliwa na visa vya ujambazi na uhalifu Kwa kipindi kirefu

‎Waziri Murkomen amesema operesheni za kikosi hicho zimechangia kuboresha usalama katika maeneo yaliyoathiriwa na shughuli za majambazi na magenge yenye silaha.

‎Amesema juhudi za maafisa hao zimewezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku kwa utulivu, huku serikali ikiendelea kuimarisha usalama katika maeneo yaliyoathiriwa.

‎Aidha  amewataka maafisa wa usalama kuendelea kushirikiana na wananchi na viongozi wa eneo hilo katika kukabiliana na uhalifu na kudumisha amani ya kudumu katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa