You are currently viewing BEI ZA KUSALIA ZILEZIL HADI AGOSTI 14

BEI ZA KUSALIA ZILEZIL HADI AGOSTI 14

Maamlaka ya kudhibiti bei za mafuta na kawi EPRA, imewahakikishia wakenya kuhusu kufanya kipaumbele maslahi ya wateja ili kuhakikisha kwamba hawaathiriwi na mabadiliko ya bei za mafuta. Ni kutokana na hali hii ambapo bei za mafuta zitasalia zilezile hadi Agosti tarehe 14 ambapo maamlaka hiyo itatoa maelekezo zaidi kuhusiana na bei za mafuta.

Ikumbukwe hapo awali kupandishwa kwa bei ya mafuta kulichangia mgomo wa wahudumu wa matatu hali iliyo ilazimu serikali kuingilia kati uku Rais William Ruto mwezi Aprili, akitangaza kupunguza kodi ya thamani ya ziada yaani VAT, kwa bidhaa za mafuta kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8 kwa kipindi cha miezi mitatu, ili kuwalinda wakenya na bei ya juu ya mafuta.