Mbunge wa Kesses, CPA Julius Rutto, amesema uhaba wa mita za umeme nchini unatokana na sintofahamu kuhusu taasisi inayopaswa kununua vifaa hivyo kati ya Kenya Power na shirika la kusambaza umeme vijijini REREC.
Ruto amesema hali hiyo imeathiri utekelezaji wa mpango wa Last Mile Connectivity, huku wananchi wengi wakishindwa kuunganishiwa umeme licha ya miundombinu kukamilika katika baadhi ya maeneo.
Ameitaka wizara ya kawi kuweka wazi majukumu ya kila taasisi ili kuondoa mkanganyiko na kuharakisha usambazaji wa mita kwa wananchi. Hoja hiyo imeibuliwa wakati kamati ya bunge ya nishati ikiendelea kuchunguza sababu za kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi ya kuunganisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

