Mwakilishi wa wadi ya Tirioko, Lokales Sam, ambaye amemtaka waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, kuingilia kati na kuhakikisha masoko yaliyofungwa katika eneo la tiaty kutokana na operesheni za kiusalama yanafunguliwa tena.
Lokales amesema kufungwa kwa masoko hayo kumedhoofisha pakubwa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo, huku wafanyabiashara, wakulima na wafugaji wakikosa sehemu ya kuuza bidhaa zao na kujipatia kipato.
Aidha amesisitiza kuwa kufunguliwa kwa masoko kutasaidia kufufua uchumi wa tiaty na kuboresha maisha ya wakazi wanaotegemea biashara za kila siku kama chanzo kikuu cha mapato.

