You are currently viewing SERIKALI YAHIMIZWA KUJIANDAA KIKAMILIFU KWA KIPINDI KIGUMU CHA BAA LA NJAA KUFUATIA KUANGAMIA KWA MAZAO SHAMBANI KUTOKANA NA UKOSEFU WA MVUA

SERIKALI YAHIMIZWA KUJIANDAA KIKAMILIFU KWA KIPINDI KIGUMU CHA BAA LA NJAA KUFUATIA KUANGAMIA KWA MAZAO SHAMBANI KUTOKANA NA UKOSEFU WA MVUA

Mwaniaji wa kiti cha uwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Baringo,Rebecca Lomong, ameihimiza serikali kuanza maandalizi ya kukabiliana na uwezekano wa uhaba wa chakula kufuatia miezi kadhaa ya kukosekana kwa mvua iliyoshuhudiwa katika kaunti hiyo.

‎Lomong ametoa wito kwa serikali ya Kitaifa na ile ya Kaunti kuweka mikakati ya dharura, ikiwemo usambazaji wa mbegu zinazostahimili ukame, msaada wa chakula kwa familia zilizoathirika na kuimarisha programu za usalama wa chakula.

Aidha, amewataka wakazi wa kaunti ya Baringo kutumia mbinu bora za kuhifadhi chakula na kukumbatia kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi ili kupunguza athari za ukame. Amesisitiza kuwa maandalizi ya mapema yatasaidia kuzuia mzozo wa chakula na kulinda maisha pamoja na ustawi wa wananchi.