You are currently viewing GACHAGUA AJIPIGIA DEBE KUPEPERUSHA BENDERA YA UPINZANI

GACHAGUA AJIPIGIA DEBE KUPEPERUSHA BENDERA YA UPINZANI

Kinara wa chama cha DCP, Rigathi Gachagua, amesema ana uwezo na  nafasi nzuri zaidi katika upande wa upinzani  kumng’oa rais William Ruto mamlakani.

Gachagua amesema anaamini ana uwezo wa kuunganisha upinzani na kutoa changamoto kubwa kwa serikali katika uchaguzi ujao.

Wakati huo uo, viongozi wengine wa chama cha DCP wamewakosoa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani kwa kile walichokitaja kuwa ni kumdharau kinara wao, rigathi gachagua.

Viongozi hao wamesisitiza kwamba Gachagua anapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa kama mmoja wa viongozi wakuu katika siasa za upinzani nchini.