You are currently viewing IDARA YA UTABIRI WA HALI YA ANGA YATOA TAARIFA KWA UMMA

IDARA YA UTABIRI WA HALI YA ANGA YATOA TAARIFA KWA UMMA

Idara ya utabiri wa hali ya anga, imetangaza kwamba sehemu nyingi humu nchini, zitakumbwa na hali ya hewa kavu katika kipindi cha saa 24 zijazo, japo mvua inatarajiwa katika sehemu za Nairobi, Magharibi ya nchi na Nyanda za Juu za Kati.

Idara hiyo imesema hali ya ukame itatawala katika sehemu kubwa ya nchi, uku kaunti chache tu zikitarajiwa kupata mvua.

Kulingana na utabiri huo mvua inatarajiwa katika sehemu za kaunti ya Nairobi, Bungoma, Kisii, Kericho, Kisumu, Nyamira, Migori, Nyeri, Nyandarua na Trans Nzoia.

Idara hiyo pia imesema kwamba, kutashuhudiwa kwa mvua katika maeneo mengine ya kaunti za Embu, Meru, Uasin Gishu, Nandi, Siaya, Homabay, Nakuru, Narok, Kakamega na Busia.

Wakaazi katika maeneo ya Kati na Kusini Mashariki aidha wamesahuriwa kutarajia hali ya baridi na mawingu ya mara kwa mara. Maeneo hayo yanajumuisha kaunti za Nairobi, Kiambu, Embu, Kirinyaga, Laikipia, Meru, Murang’a, Nyandarua, Nyeri, Tharaka Nithi, Kitui, Machakos, Kajiado na Makueni.

Idara hiyo ya utabiri wa hali ya anga vilevile imeonya zaidi kuhusu upepo mkali katika sehemu za kaunti za Lamu, Kilifi, Garrisa, Wajir na Marsabit. Upepo mkali unaweza kuathiri shughuli za baharini kando ya sehemu za Pwani.

Idara ya utabiri wa hali ya anga pia imewashauri wananchi kuendelea kufuatilia taarifa rasmi kuhusu hali ya hewa, kupitia tuvuti yake na majukwa mengine rasmi, kwani hali inaweza kuendelea kubadilika.