Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, amelaani vikali visa vya utekaji nyara cha hivi punde chake mwanahabari Alex Kiprotich, huku akitaja tukio hilo kuwa la aibu na la kinyama.
Murkomen ameitaka idara husika kufanya uchunguzi wa haraka na kuhakikisha wote waliohusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani,
akimtaka Inspekta Jenerali wa polisi, Douglas Kanja, kuimarisha usalama wa wanahabari, hasa kuelekea kipindi cha uchaguzi.
Murkomen amesema serikali imejitolea kulinda uhuru wa vyombo vya habari na kuhakikisha wanahabari wanaweza kutekeleza majukumu yao bila vitisho au hofu.

