You are currently viewing KEPSHA YASHANGAZWA NA UCHIMBAJI WA DHAHABU KATIKA UWANJA WA SHULE TURKANA

KEPSHA YASHANGAZWA NA UCHIMBAJI WA DHAHABU KATIKA UWANJA WA SHULE TURKANA

Viongozi wa Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi nchini (KEPSHA) katika Kaunti ya Turkana wameshangazwa na hatua ya baadhi ya wakazi kuingia katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Nareng Emunyen, Turkana Kusini, na kuanza kuchimba dhahabu.

Viongozi hao wamesema shughuli hiyo ya uchimbaji madini katika uwanja wa shule inahatarisha usalama wa wanafunzi na walimu, mbali na kuathiri mazingira ya kujifunzia.

Wamezitaka mamlaka husika kuingilia kati na kuchukua hatua za haraka kukomesha shughuli hiyo, wakisisitiza kuwa uwanja wa shule unapaswa kulindwa na kutumika kwa shughuli za kielimu pekee.

APERIT FM,HII NI YETU