You are currently viewing KMPDU YATISHIA KUGOMA HIVI KARIBUNI

KMPDU YATISHIA KUGOMA HIVI KARIBUNI

Chama cha madaktari nchini KMPDU, kimetishia kugoma iwapo serikali za kaunti hazitatekeleza nyongeza ya mishahara, kulipa malimbikizi ya madeni na kutekeleza kikamilifu mkataba wa makubaliano ya pamoja, wa mwaka 2017-2021.

Katibu mkuu wa KMPDU Davji Attelah, amewaagiza madaktari katika kaunti zote 47, kukagua mishahara yao ya Julai mwaka 2026, ili kubainisha iwapo viwango vipya vya mishahara vimetekelezwa.

Ameonya kuwa kaunti zitakazo shindwa kutekeleza makubaliano hayo, zitakabiliwa na mgomo wa madaktari pamoja na hatua za kisheria dhidi ya maafisa husika.

KMPDU imesema imekamilisha njia zote za mazungumzo ya taratibu za kisheria, uku ikieleza kuwa hakuna sababu ya kuendelea kuchelewesha utekelezwaji wa CBA, nyongeza ya mishahara na malipo ya madeni ya awali.

Attelah amesisitiza kuwa madaktari wako tayari kuchukua hatua za pamoja iwapo serikali za kaunti hazitatekeleza makubaliano mara moja.