You are currently viewing SERIKALI KUWASILISHA MAPENDEKEZO YAKE KUHUSU MPANGO WA MABADILIKO YA KIUCHUMI KUPITIA RUWAZA YA MWAKA 2060

SERIKALI KUWASILISHA MAPENDEKEZO YAKE KUHUSU MPANGO WA MABADILIKO YA KIUCHUMI KUPITIA RUWAZA YA MWAKA 2060

Rais William Ruto leo ataongoza serikali kuwasilisha mapendekezo yake kuhusu mpango wa mabadiliko ya kiuchumi kupitia ruwaza ya 2060 katika jumba la mikutano la KICC Jijini Nairobi.

Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha takriban wakenya elfu tano, kutoka kaunti zote 47, pamoja na wawakilishi wa Mihimili ya serikali, Bunge pamoja na Mahakama.

Waziri wa fedha John Mbadi amesema mkutano huo utakuwa mwanzo wa ushirikishwaji wa umma, ambapo wakenya watatoa maoni yatakayo saidia kuanzisha dira ya maendeleo ya nchi kuelekea mwaka 2060.

Mbadi amesema ruwaza ya mwaka 2060, si mpango wa rais Ruto pekee, akiwataka wakenya kuwasilisha mapendekezo ya kuhusu namna nchi inavyoweza kufikia hadhi ya mataifa yaliyo stawi zaidi kiuchumi ndani ya miaka 25 pekee.

Baada ya maoni ya wananchi kukusanywa mpango huo unatarajiwa kuandaliwa na kuwasilishwa bungeni kama mswada.

Iwapo utaidhinishwa na bunge la kitaifa na seneti, msawada huo utawasilishwa kwa rais Ruto hili kuidhinishwa kwa lengo la kuweka mpango huo katika msingi wa kisheria.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa pia kuweka mwelekeo wa maendeleo ya Kenya baada ya ruwaza ya mwaka 2030, yakilenga kuimarisha taasisi kukuza rasilimali watu na kuhakikisha maendeleo jumuishi.

                                                                                                                    APERIT FM, HII NI YETU