You are currently viewing LAGAT ATEMA MOTO KWA WAHUNI NA WAGEMAJI

LAGAT ATEMA MOTO KWA WAHUNI NA WAGEMAJI

Naibu Inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat, ameta onyo kali kwa makundi ya wahuni, akisema yatakabiliwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika eneo la Moi’s Bridge kaunti ya Uasin Gishu, Lagat amesema vyombo vya usalama vimejipanga kuhakikishia vitendo vya ujambazi, uhalifu na uhuni, hazitaathiri shughuli za kijamii na uchumi.

Lagat amesisitiza kuwa polisi wataendelea kuimarisha doria na oparesheni katika maeneo mbalimbali nchini, ili kukabiliana na makundi ya wahalifu, na kuwahakikishia usalama wa wananchi na mali zao.

Aidha amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama, kwa kutoa taarifa kuhusu uhalifu, akisema ushirikiano huo ni muhimu katika kuzuia na kupambana na uhalifu nchini.

Vilevile, Lagat pia amewatahadharisha wagemaji na wauzaji wa pombe haramu na dawa za kulevya eneo hilo.