Mbunge wa Sigor kaunti ya Pokot Magharibi, Peter Lochakapong, akishirikiana na kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maendeleo ya bonde la kerio (KVDA), Moses Kipchumba, wameongoza zoezi la ugavi wa Ngamia 100 kwa familia mbalimbali katika eneo la Masol, Kaunti ya Pokot Magharibi
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, kaimu mkurugenzi mkuu wa kvda amesema mpango huo unalenga kusaidia jamii zinazoishi katika maeneo kame na nusu kame ambayo yameathiriwa na ukame. Ameeleza kuwa kuanzishwa kwa ufugaji wa ngamia ni mkakati wa kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza kipato cha familia na kujenga ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wake, Mbunge Peter Lochakapong amewahimiza wanufaika kuwatunza vizuri ngamia hao ili waweze kuboresha maisha yao na kuchangia maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.

