Aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Pokot Magharibi na kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Samuel Poghisio amewasuta viongozi wa kisiasa nchini kwa kuelekeza nguvu zao katika kuhakikisha wanapata nafasi ndani ya serikali badala ya kutetea maslahi ya wananchi waliowachagua
Kwenye mahojiano na runinga moja nchini Poghisio amesema hali hiyo imesababisha taifa kugawanywa kwa misingi ya kikabila jambo ambalo ametaja kudhoofisha maendeleo na umoja wa kitaifa
Aidha ameelezea masikitiko yake kutokana na mtindo mpya wa kampeni za mapema na vurugu za kila baada ya uchaguzi ambao umekiti mzizi humu nchini akisema hali hiyo inayumbusha mfumo wa demokrasia ambao umekuwa ukipigiwa mfano na mataifa tofauti Barani Afrika na duniani

