Wanaharakati na makundi ya kutetea haki za kibinadamu, sasa yanawataka wakenya kutoka matabaka mbalimbali kujitokeza kushiriki maandamano ya Sab Saba. Wanaharakati hao wamesema watatembea hadi katika bunge la kitaifa, wakilalamikia visa vya kutekwa nyara na mauaji ya kiholela yanayotekelezwa na polisi.
Aidha wamesema tayari wamearifu maafisa wa polisi kuhusiana na maandamano hayo, wakisema yatakuwa ya amani.
Kihistoria Saba Saba inahusishwa na maandamano yaliyofanyika tarehe saba Julai mwaka wa 1990, ambapo wanaharakati na viongozi wa upinzani walishinikiza kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa pamoja na mageuzi ya kidemokrasia hapa nchini.
Maandamano hayo yaliongozwa na Kenneth Matiba na Charles Rubia, miongoni mwa viongozi wengine walio pigania demokrasia.
Katika miaka ya hivi karibuni saba saba utambuliwa na wengi kuwa siku ya kutafakari kuhusu demokrasia, haki za kiria, utawala bora na uhuru wa kisiasa nchini Kenya.

