You are currently viewing SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAPOKEA DAWA YENYE KIMA CHA SHILINGI MILIONI 81 KUTOKA KEMSA

SERIKALI YA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAPOKEA DAWA YENYE KIMA CHA SHILINGI MILIONI 81 KUTOKA KEMSA

Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi imezindua rasmi usambazaji wa    shehena ya kwanza ya dawa na vifaa vya matibabu katika   robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 kuelekezwa katika vituo 173 kote kaunti hiyo

Kulingana na Kachapin  hatua hiyo inalenga kuhakikisha dawa, vifaa na bidhaa nyingine muhimu za afya zinafikia vituo vya afya kwa wakati, ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi,na  kupunguza changamoto ya uhaba wa dawa na vifaa katika vituo vya afyan

Aidha gavana Kachapin amesisitiza umuhimu wa usimamizi bora wa bidhaa hizo ili kuhakikisha zinawafikia wanaozihitaji kwa wakati

Vilevile ameonya kuhusu visa vya wizi wa dawa akitoa wito wa uadilifu na uwajibikaji katika mchakato mzima

Wakati huo uo ameelezea dhamira yake ya kuendelea kuimarisha huduma za afya huku akitolea mfano uajiri wa wahudumu wa afya na uboreshaji wa vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanafaidi kikamilifu na huduma kwenye kaunti hiyo badala ya kuzuru zingine jirani

APERIT FM,HII NI YETU