Mji wa Lodwar na maeneo ya jirani katika kaunti ya Turkana yanatarajiwa kuunganishwa na gridi ya taifa ya umeme kwa mara ya kwanza tangu kenya ijipatie uhuru.
Kulingana na baadhi ya maafisa wa serikali ,kampuni ya Kenya Power iko katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa kituo cha kusambaza umeme mjini humo yenye kilowati 66 yenye urefu wa kilomita 90 kutoka Lokichar hadi Lodwar.
Wamesema miradi hiyo miwili inayofadhiliwa na serikali imegharimu jumla ya shilingi bilioni moja na milioni kumi.
Ikumbukwe kuunganishwa kwa Lodwar na gridi ya taifa kunatarajiwa kuboresha upatikanaji wa umeme unaoaminika na kusaidia shughuli za kiuchumi, biashara, huduma za kijamii na maendeleo katika kaunti ya Turkana vilevile kufungua fursa zaidi za uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi katika eneo hilo.
APERIT FM,HII NI YETU

