You are currently viewing MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO ENEO LA O-LKALAU YAIPA SERIKALI CHANGAMOTO KUJITUMA ZAIDI

MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO ENEO LA O-LKALAU YAIPA SERIKALI CHANGAMOTO KUJITUMA ZAIDI

Mbunge wa Tiaty   William Kassait Kamket, amesema matokeo ya uchaguzi mdogo wa Ol-Kalou yameimarisha nafasi ya eneo la Mlima Kenya Mashariki  ndani ya serikali ya Kenya Kwanza, akidai kuwa matokeo hayo yameonyesha mwelekeo mpya wa kisiasa katika eneo hilo.


‎Kamket amesema ushindi huo unatoa fursa kwa viongozi wa eneo hilo kuimarisha ushirikiano wao na serikali ya Rais William Ruto ili kuhakikisha wananchi   wananufaika zaidi na miradi ya maendeleo na huduma za serikali.


 Kamket ameongeza kuwa mshikamano wa kisiasa na ushirikiano kati ya viongozi wa kitaifa na wa maeneo mbalimbali utasaidia kuimarisha utulivu wa kisiasa na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi huku akiwataka viongozi kuepuka siasa za migawanyiko na badala yake kujikita katika masuala yanayowaletea wananchi maendeleo.