Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC, imeorodhesha rasmi viwango vya juu vya matumizi ya fedha za kampeni, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Kwa mujibu wa IEBC, mgombea wa urais ataruhusiwa kutumia hadi shilingi bilioni 6.1, uku vyama vya kisiasa vikipewa kikomo cha matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 24.
Kuhusu nyadhifa za Ugavana, Useneta na Uwakilishi wa kike, Nairobi imepewa kiwango cha juu zaidi cha matumizi cha hadi shilingi milioni 181, Turkana unafuata kwa shilingi milioni 142, uku Marsabiti, Wajir na Kiambu, vikifuata kwa viwango vya juu vya matumizi ya fedha za kampeni.
Katika nafasi ya ubunge North Hor ndio imepewa kiwango cha juu zaidi cha shilinigi milioni 100, uku Wundanyi ikiwa na kiwango cha chini cha takriban shilingi milioni 15.
Kwa nafasi ya mwakilishi wadi, wadi ya Tarbi, katika kaunti ya Marsabit imepewa kiwango cha juu zaidi cha matumizi cha zaidi ya shilingi milioni 22.
IEBC imesema fedha hizo zitatumika katika shughuli zilizo idhinishwa kama vile matangazo, usafiri, malipo ya wafanyikazi wa kampeni, mikutano, mawasiliano, usalama, malazi pamoja na gharama zingine halali za kampeni.
Kipindi cha matumizi ya fedha za kampeni, kitaanza miezi 6 kabla ya uchaguzi mkuu, na kumalizika siku 14 baada ya uchaguzi.
APERIT FM, HII NI YETU

