Waziri wa mazingira na misitu, Deborah Mulongo, amewataka wakenya kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza katika kaunti hii ya Trans-Nzoia, waziri Mulongo amesema kuwa hadi sasa taifa la Kenya limepanda miti zaidi ya Bilioni 1.9 kwa kipindi kifupi. Ameongeza kuwa Kenya iko katika safu ya mbele kimataifa katika utunzaji wa mazingira.
Waziri Mulongo amewataka vijana kujitegemea kimaisha. Amesema badala ya kutumika na viongozi wa kisiasa kuzua vurugu katika kipindi hiki, vijana wanafaa kufungua biashara ndogo ndogo za kujiendeleza badala ya kutegemea pesa za wanasiasa.

