Gianni Infantino ameitisha mkutano wa dharura wa watumishi wa FIFA mjini Rabat Jumatano. Hii ni kufuatia matamshi ya Arsene Wenger yaliyoongeza shinikizo kwa rais huyo.
Hii ni kufuatia matamshi ya Arsene Wenger yaliyoongeza shinikizo kwa rais huyo. Kocha wa zamani wa Arsenal, Wenger, ambaye sasa ni mkuu wa kitendo cha FIFA cha maendeleo ya soka duniani, alitoa taarifa akisema “hakuhusika” katika mpango wa kutafuta uwekezaji binafsi katika kampuni ya kuendesha Kombe la Dunia lakini kwamba uamuzi wa kuuondoa mpango huo ulikuwa “wa lazima kabisa na usiokuwa na swali”.
Shirika la Habari la AP linasema mkutano huo nchini Morocco uliitishwa baada mapema wiki hii na pia utawajumuisha katibu mkuu Mattias Grafstrom na bodi ya usimamizi wa FIFA, ambayo inajumuisha mkuu wa watumishi wa shirikisho hilo Daniel O’Toole, afisa mkuu wa sheria Emilio Garcia Silvero, mkuu wa vyama wanachama Elkhan Mammadov, mkuu wa Rasilimali Watu Kimberly Morris, mkurugenzi wa vyombo vya habari Bryan Swanson na mkurugenzi wa mawasiliano David Farrelly.
APERIT FM, HII NI YETU

