You are currently viewing RAIS RUTO ATOA HAKIKISHO LA KUANDALIWA UCHAGUZI HURU NA HAKI MWAKA UJAO

RAIS RUTO ATOA HAKIKISHO LA KUANDALIWA UCHAGUZI HURU NA HAKI MWAKA UJAO

Rais William Ruto amewahakikishia wakenya kuwa uchaguzi mkuu wa 2027 utafainyika kwa amani akisisitiza kuwa serikali haitaruhusu ghasia kabla wakati na baada ya uchaguzi huo.

Akizungumza katika kaunti ya Busia Rais Ruto amesema tofauti za kisiasa, hazipaswi kuhatarisha amani ya taifa akiwataka wakenya kudumisha utulivu bila kujali misimamo yao ya kisiasa.

Ameonya kuwa serikali itachukua hatua kali dhidi ya wahuni wote na kuhakikisha kila mwanasiasa anafanya shughukli zake kwa amani bila kuvamiwa.