Mbunge wa Kapseret, Oscar Kipchumba Sudi, ametoa wito kwa jamii ya Kalenjin kuimarisha umoja na mshikamano, akisisitiza kuwa siasa za mgawanyiko kati ya maeneo ya North Rift na South Rift zinapaswa kukomeshwa.
Sudi ambaye ni kinara wa wanamuziki wa jamii ya Kalenjin, amesema tofauti za kikanda zimekuwa zikidhoofisha sauti ya jamii ya kalenjin na kuchelewesha maendeleo, akieleza kuwa viongozi wanapaswa kuacha siasa zinazochochea migawanyiko na badala yake kuunganisha wananchi ili kushughulikia changamoto zinazowakabili.
Aidha amesisitiza kuwa maendeleo ya jamii hayawezi kupatikana ikiwa kutakuwa na migawanyiko ya kisiasa na kikanda huku akiwataka viongozi kushirikiana bila kujali wanatoka eneo gani, huku akibainisha kuwa umoja ndiyo msingi wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Sudi pia amewahimiza vijana na wananchi kwa ujumla kuendeleza amani na mshikamano, akisema kizazi cha sasa kina jukumu la kujenga jamii iliyo na umoja na yenye uwezo wa kunufaika na fursa za maendeleo

