You are currently viewing MVUA, BARIDI NA UKAME KWENYE MIZANI

MVUA, BARIDI NA UKAME KWENYE MIZANI

Idara ya utabiri wa hali ya Anga imetangaza kuwa maeneo mengi ya nchi inchini, yataendelea kushuhudia ukavu na ukame baina ya Agosti 13 na terehe 20 ya mwezi huu, uku kaunti 8 pekee zikitarajiwa kuwa na mvua.

Kulingana na taarifa ya idara hiyo, kaunti za Bungoma, Trans-Nzoia, Nakuru, Uasin-Gishu, Elgeiyo Marakwet, Kericho, Nyandarua na Nyeri, uwenda kukawa na mvua katika kipindi hicho, uku sehemu kubwa ya nchi ikisalia bila mvua.

Utabiri huo unaziweka kaunti 8 kuwa miongoni mwa kaunti ambazo zinatarajiwa kuwa na mvua katika kipindi hicho, uku kaunti zingine zikiwa na hali ya baridi na mawingu.

Baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuwa na baridi na mawingu, ni yakiwamo Embu, Kiambu, Kirinyaga, Laikipia, Nairobi, Meru, Nyandarua, Nyeri, Tharaka Nithi, Nakuru, Machakos, Taita Taveta, Marsabit na Wajir.

Kaunti za Nyandarua, Nyeri na Nakuru, aidha zimejumuishwa katika makundi yote mawili, zikitarajiwa kuwa na mvua, pia kushuhudiwa kwa hali ya baridi.

Aidha kaunti zilizo katika hatari kubwa, zimehimizwa kuweka mikakati ya mapema kujianda kwa mvua ya El-Nino inayotarajiwa kati ya msimu wa Oktoba, Novemba na Disemba.

Kaunti zilizopo hatarini ni zikiwapo Homabay, Kisumu, Nakuru, ambako viwango vya maji katika maziwa Victoria, Turkana, Baringo, Bogoria, Elmentaita, Navasha na Nakuru tayari vimeanza kuongezeka.

                                                                                                                      APERIT FM, HII NI YETU