You are currently viewing SIASA NI KWA MUDA TU! TAIFA KIPAUMBELE, ASEMA KINDIKI

SIASA NI KWA MUDA TU! TAIFA KIPAUMBELE, ASEMA KINDIKI

Naibu wa rais Prof. Kithure Kindiki, ameendelea kutoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuepuka kauli zinazoweza kuhatarisha mshikamano wa kitaifa.

Kindiki amesema ushindani wa kisiasa haupaswi kuvuruga amani, akiwataka viongozi na wananchi kujikita katika siasa za hoja na ustaarabu licha ya tofauti zao za kisiasa.

Akizungumza uko Mrang’a, Kindiki amesema siasa ni ushindani wa muda, na kwamba hiafai kuwa chambo cha kuchochea uhasama miongoni mwa wakenya.

Amesema viongozi wanao wanaia nafasi za kisiasa, wanapaswa kupimwa kwa rekodi zao za utendaji badala ya misingi ya ukabila au maeneo wanayotoka.

                                                                                                              APERIT FM, HII NI YETU