Gavana wa Elgeyo-Marakwet, Wisley Rotich, amesema kuwa vituo vya afya vya umma katika kaunti hiyo havikabili tena tatizo la mara kwa mara la ukosefu wa dawa.
Rotich amesema serikali ya kaunti imeweka mfumo wa ufuatiliaji wa upatikanaji wa dawa unaomwezesha yeye pamoja na maafisa wa afya kupata taarifa mara moja iwapo dawa fulani imeanza kupungua au kumalizika katika kituo chochote
Mfumo huo una umuhimu mkubwa kwa sababu changamoto ya dawa imekuwa ikihusishwa si tu na kukosekana kwa dawa, bali pia na kuchelewa kwa usambazaji na vituo kupokea dawa tofauti na zile walizoagiza.
Mwaka 2023, Rotich alikiri kwamba baadhi ya vituo vilikuwa havipokei dawa kwa wakati, huku vingine vikipokea dawa ambazo havikuagiza ,Hivyo, mfumo unaotajwa sasa unaonekana kuwa sehemu ya juhudi za kubadilisha mfumo wa kusubiri kituo kuripoti tatizo baada ya dawa kuisha, kwenda kwenye mfumo wa kutambua tatizo mapema na kuchukua hatua kabla ya upungufu kuwa mkubwa.
APERIT FM,HII NI YETU

