You are currently viewing NAMOIT AISHINIKIZA SERIKALI KUHAKIKISHA WANABODABODA WANALINDWA DHIDI YA MATAPELI

NAMOIT AISHINIKIZA SERIKALI KUHAKIKISHA WANABODABODA WANALINDWA DHIDI YA MATAPELI

Mbunge wa Turkana Kusini,   John Ariko Namoit, ametoa wito wa kuchukuliwa   hatua za haraka kulinda sekta ya boda-boda dhidi ya kampuni za mikopo anazodai zinawanyanyasa wanabodaboda

Dkt. Namoit amesema baadhi ya kampuni za utoaji mikopo zimekuwa zikiweka waendesha boda-boda katika hali ngumu kwa kuwapa mikopo ya kununua pikipiki, lakini baadaye kuwanyang’anya pikipiki hizo wanaposhindwa kukamilisha malipo yao

 Ariko   amesema hali hiyo inawaweka wahudumu hao  katika mazingira magumu ikizingatiwa  pikipiki ndiyo chanzo chao kikuu cha mapato  

 ameitaka serikali kuchukua hatua kuhakikisha kuwa kampuni zinazotoa mikopo kwa waendesha boda-boda zinafanya shughuli zao kwa uwazi, bila kuwanyonya wananchi wanaotegemea mikopo hiyo kujiajiri.

APERIT FM,HII NI YETU