Wakenya uwenda wakakumbana na ongezeko la bei ya mafuta kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta gafi katika soko la kimataifa uku maamlaka ya kudhibiti kawi EPRA ikitarajiwa kutangaza mapitio mapya ya bei za mafuta Julai 14.
Bei ya mafuta aina ya Brent Crude ambayo kenya utumia kama kigezo cha kupanga bei ya mafuta yanayo agizwa kutoka nje, imeongezeka kwa takriban asilimia 5 kutokana na mvutano mpya kati ya Marekani na Iran.
Ongezeko hilo limechochewa na mashambulio ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Iran, kufuatia madai kuwa Terhan ilihusika na mashambulio dhidi ya meli za kibiashara katika Mlango wa Bahari wa Hormuz, njia muhimu inayopitisha sehemu kubwa ya mafuta yanayo safirishwa duniani.
Wataalamu wa sekta ya kawi wanaonya kuwa, endapo hali iyo itaendelea, usambazaji wa mafuta unaweza kutatizika na kusababisha bei kuendelea kupanda katika soko la kimataifa.
Kenya ambayo utegemea uwagizaji wa mafuta kutoka nje, kupanda kwa bei ya mafuta gafi kunaweza kusababisha ongezeko la bei za mafuta katika vituo vya kuuza mafuta, hali itakayoongeza gharama za usafiri na maisha kwa ujumla.

