Maeneo mbalimbali nchini yatashuhudia mchanganyiko wa mvua, ngurumo za radi na vipindi vya jua kuanzia leo Julai 28 hadi Agosti 3 mwaka huu.
Idara ya utabiri wa hali ya anga imetabiri kuwa maeneo ya Magharibi ya Kenya, Bonde la Ufa na sehemu za Mlima Kenya zinatarajiwa kupokea mvua kubwa zaidi.
Mvua za asbuhi zimetabiriwa katika kaunti za Siaya, Busia, Bungoma, Kakamega, Uasin Gishu na Turkana, uku maeneo mengine yakishuhudia mawingu na mvua nyepesi.
Idara iyo pia imesema mvua za alasiri zikiambatana na ngurumo za radi, zianatarajiwa katika kaunti kadhaa zikiwamo Nairobi, Nakuru, Kisumu, Kericho, Nandi, Narok, Meru, Embu, Kiambu, Nyeri, Nyandarua, Laikipia, Trans -Nzoia, Turkana, Bungoma, Busia, Kakamega, Homabay, Migori pamoja na kaunti ya Vihiga.
Hata hivyo kaunti za Garrisa, Isiolo, Kajiado, Kilifi, Kitui, Kwale, Lamu, Machakos, Makueni, Mandera, Marsabit, Mombasa, Samburu, Taita Taveta, Tana River na Wajir, zinatarajiwa kuwa na vipindi virefu vya jua hasa nyakati za alasiri.
Idara ya hali ya anga sasa imewaonya wakaazi wa maeneo yanayo tarajiwa kushuhudia ngurmo za radi ikiwataka waendelee kufuatilia taarifa za hali ya anga na kuchukua tahadhari zinazo stahili.
Wakati huo huo kaunti za Homabay, Kisumu na Nakuru, zimehimizwa kujiandaa mapema kwa mvua za El-Nino zinazo tarajiwa kati ya miezi za Oktoba na Disemba mwaka huu.
Wataalamu wa hali ya anga wameonya kuwa mvua hizo zinaweza kusababisha maafuriki makubwa na kuongezeka kwa kina cha maji katika maziwa kadhaa nchini, zikiwamo Victoria, Naivasha, Baringo na Nakuru, hali inayoweza kuhatarisha maisha pamoja na mali.

