Rais William Ruto amesema kuwa ujenzi wa barabara zote zilizokuwa zimekwama sasa umeanza tena katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza kwenye ibada ya Jumapili Mjini Eldoret ,Rais Ruto amesema kaunti ya Uasin Gishu inanufaika na ujenzi wa mtandao wa barabara mpya zenye urefu wa kilomita 500 zinazowekwa lami, hatua anayosema itarahisisha usafiri, kuchochea biashara na kuboresha shughuli za kiuchumi katika kaunti hiyo.
Rais amesisitiza kuwa serikali imejizatiti kuhakikisha miradi yote ya miundombinu iliyokwama inakamilishwa kwa wakati ili wananchi wapate huduma bora na maendeleo yaweze kufikiwa katika sehemu zote za nchi.
Aidha ametoa hakikisho la kuunganishwa kwa umeme kwenye makaazi na vijiji mbalimbali kupitia mpango wa last mile connectivity kwa kubainisha kwamba hazina maalum ya miundo mbinu iliyobuniwa itasaidia kupiga jeki mpango huwo

