You are currently viewing ASENALI YAZIDI KUJIANDAA

ASENALI YAZIDI KUJIANDAA

Mchezajiw a klabu ya Asenali Jurrien Timber ameondoka kambini nchini Hispania kwa miadi iliyokuwa imepangwa awali jijini London kama sehemu ya mpango wake wa matibabu ya majeraha ya nyonga (groin).

Klabu ya Asenali imesisitiza kuwa si kurudi nyuma kwa hali yake, na anatarajiwa kurejea kambini baadaye.

Aidha kocha wa klabu hiyo Mikel Arteta amesema kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita hakupaswi kuwa mwisho wa mafanikio, bali mwanzo wa kipindi cha mafanikio makubwa. Amesema kiwango cha ubora kinapaswa kuwa utamaduni wa klabu.

Hata hivyo mshambuli wa Real Madrid Vinícius Júnior aliyekuwa anamezewa mate na klabu ya Asenali, anaonekana kubakia kwenye timu hiyo ya Real Madrid. Klabu hiyo haina mpango wa kumuuza na ina imani atakubali kusaini mkataba mpya, licha ya Arsenal kuonyesha nia kwa dhati ya kumsajili.

Kutokana na hali hiyo, AsenalI inaendelea kufuatilia Bradley Barcola wa PSG na Julián Alvarez wa Atlético Madrid kama mbadala. Hata hivyo, Barcola anakadiriwa kugharimu takribani pauni milioni 145, huku Atlético ikiwa haitaki kumuuza Alvarez.

AsenalI pia inatajwa kuendelea kuvutiwa na Bruno Guimarães wa Newcastle, ingawa Newcastle imesisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi.