Mkuu wa utumishi wa umma, Felix Koskei, amewataka wakenya kushiriki kikamilifu katika mazungumzo ya kitaifa yanayolenga kuunda ajenda ya maendeleo ya kenya baada ya mwaka 2030.
Koskei amesema mazungumzo hayo yanapaswa kuangalia mustakabali wa taifa kwa muda mrefu, huku mipango ya maendeleo ikifikishwa hadi mwaka 2060 au 2063, mwaka ambao kenya itakuwa imetimiza miaka 100 tangu kupata uhuru.
Amesema ushiriki wa wananchi ni muhimu katika kuamua vipaumbele vya taifa, kuhakikisha mipango ya maendeleo ya muda mrefu inaakisi matarajio ya wakenya na vizazi vijavyo.
Amesisitiza umuhimu wa kuwa na mjadala mpana na jumuishi kuhusu aina ya kenya ambayo wananchi wanataka kuijenga katika miongo ijayo.
APERIT FM,HII YETU

