Mbunge wa Endebess, Robert Pukose, anataka ombi la wananchi dhidi ya kampuni ya safaricom kushughulikiwa upesi, kufuatia madai ya ukiukaji wa usalama wa data za wateja.
Dkt. Pukose amesema baadhi ya wananchi wanaendelea kupokea ujumbe mfupi na simu kutoka kwa watu wasiowafahamu, licha ya kutowahi kuwapa watu hao nambari zao za simu.
Ameitaka bunge na taasisi husika kuchunguza suala hilo kwa haraka, ili kubaini chanzo cha kuvuja kwa taarifa za kibinafsi na kuhakikisha data za wananchi zinalindwa.
Amesisitiza kuwa usalama wa taarifa binafsi ni haki muhimu ya kila mwananchi, na kwamba kampuni zinazoshughulikia data za wateja zinapaswa kuwajibika pale kunapokuwa na ukiukaji wa usalama wa taarifa.
APERIT FM,HII NI YETU

