You are currently viewing GAVANA BII AWATAKA WAKENYA KUANGAZIA UTENDAKAZI KWENYE UCHAGUZI UJAO VILEVILE KUZINGATIA KILIMO MSETO

GAVANA BII AWATAKA WAKENYA KUANGAZIA UTENDAKAZI KWENYE UCHAGUZI UJAO VILEVILE KUZINGATIA KILIMO MSETO

gavana wa uasin gishu, jonathan bii, amewahimiza wakazi wa kaunti hiyo kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura.

Bii amesema ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ni muhimu katika kuamua uongozi wa siku zijazo huku pia, akiwataka wakazi kuzingatia miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya utawala wa rais William   Ruto katika kaunti hiyo.

 Aidha gavana bii amesema wakulima wa mahindi katika kaunti hiyo wamekumbwa na hasara ya mazao mwaka huu kutokana na mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Bii amewahimiza wakazi kuachana na utegemezi wa zao moja na badala yake kukumbatia kilimo cha mazao mbalimbali ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesisitiza kuwa utofauti katika kilimo utawasaidia wakulima kupunguza hasara wakati zao moja linaposhindwa kufanya vizuri kutokana na hali mbaya ya hewa.

APERIT FM,HII NI YETU