Shirikikisho la Kandanda Duniani-FIFA linafikiria kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia kutoka 48 hadi 64 kuanzia mashindano ya mwaka 2030.
Mpango huo umependekezwa wakati Rais wa FIFA, Gianni Infantino, akikabiliwa na upinzani kuhusu mageuzi mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa Kombe la Dunia. Wapo wanaohofia mabadiliko hayo yataweka mbele maslahi ya kibiashara kuliko maendeleo ya mchezo.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizoripotiwa na Shirika la Press Association, FIFA inatarajia kupokea mapendekezo kutoka kwa taasisi za tathmini ifikapo Agosti 7, kufanya uamuzi Agosti 14, na kupata ripoti ya mwisho Septemba 11. FIFA bado haijatoa maoni rasmi kuhusu taarifa hizo.

