You are currently viewing KORIR ATAKA HAZINA YA MICHEZO KUBADILISHWA NA KUPEWA JINA MFUKO WA VIPAJI

KORIR ATAKA HAZINA YA MICHEZO KUBADILISHWA NA KUPEWA JINA MFUKO WA VIPAJI

Aliyekuwa Mbunge wa Cherangany,   Wesley Kipchumba Korir, amependekeza hazina ya michezo kubadilishwa na kuwa mfuko wa vipaji ili uweze kunufaisha sekta nyingine kama muziki na tasnia ya ubunifu.

Korir ametoa pendekezo hilo   katika hafla ya utoaji wa tuzo za wanamuziki wa jamii ya Kalenjin  KMFA

Amesema hatua hiyo itawawezesha wasanii na wabunifu wengine kupata ufadhili wa kukuza vipaji na kuboresha maisha yao.

Aidha, ametoa wito wa kuanzishwa kwa mfuko maalum kwa wasanii wa kalenjin ili kuwasaidia kupata huduma za kifedha, kukuza akiba na kuwekeza katika shughuli zao za kisanii.