You are currently viewing MALALAMISHI KWA FIFA BAADA YA KOMBE LA DUNIA KUKAMILIKA

MALALAMISHI KWA FIFA BAADA YA KOMBE LA DUNIA KUKAMILIKA

Shirikisho la soka nchini Norway imetangaza kuwa itawasilisha malalamiko rasmi kwa kamati ya maadili ya shirikisho la soka duniani FIFA, haya ni kufuatia uwamuzi wa kusitisha adhabu kwa mchezaji wa timu ya taifa la Marekani Folarin Balogun, ya kukosa mechi ya Kombe la Dunia.

Rais wa shirikisho la soka nchini Norway Lise Klaveness, amesema kwamba hatua hiyo imeweka uadhilifu wa michezo hatarini akidai uwamuzi huo uliafikiwa baada ya rais wa Marekani Donald Trump, kuzungumza na rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino.

Balogun alipigwa kadi nyekundu dhidi ya timu ya taifa la Bosnia na alipaswa kukosa mechi dhidi ya timu ya taifa la Ubelgiji, lakini FIFA ilisimamsha adhabu hiyo kabla ya mechi hiyo.