You are currently viewing HAKUNA KARANTINI KENYA KWA AJILI YA WAGONJWA WA EBOLA WA MAREKANI, ASEMA WAZIRI DUALE

HAKUNA KARANTINI KENYA KWA AJILI YA WAGONJWA WA EBOLA WA MAREKANI, ASEMA WAZIRI DUALE

Waziri wa afya Aden Duale, amekanusha taarifa kuwa wahudumu saba wa misaada kutoka Marekani wamewekwa kwenye Karantini ya wagonjwa wa Ebola, kilicho jengwa kwa ufadhili wa Marekani katika kambi la jeshi la anga ya Nanyuki kaunti ya Laikipia.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa kupokea Tani Tano za vifaa vya matibabu vya dharura vya kudhibiti ugonjwa wa Ebola, vilivyotolewa na serikali ya India.

Duale amesema ujenzi wa kituo hicho ulisimamishwa kufuatia amri ya Mahakama, na kwamba serikali inaheshimu utawala wa sheria.

Aidha amesema kenya bado haijarekodi kisa chochote cha Ebola, uku zaidi ya wasafiri 270 elfu, wakichunguzwa katika mipaka mbalimbali ya nchi.

Waziri Duale amesema serikali imeanzisha vituo 21 vya karantini nchini, baada ya kusimamishwa kwa ujenzi wa kituo cha Laikipia.

Hata hivyo amesisitiza kuwa serikali haita fichua maeneo ya vituo hivyo kwa kuwa hatua hiyo inaweza kuwafanya wakenya kuepuka hosipitali zinazotumika kutoa huduma hizo.