You are currently viewing KINDIKI AWATAKA MAGAVANA NA WAUGUZI KUKETI MEZANI KUSITISHA MGOMO

KINDIKI AWATAKA MAGAVANA NA WAUGUZI KUKETI MEZANI KUSITISHA MGOMO

Naibu rais Kithure Kindiki amewataka magavana na wauguzi kurejea katika meza ya mazungumzo na kutafuta suluhisho la mzozo   ambao umesababisha mgomo wa wauguzi ambao umeingia siku ya 34.

Kindiki   amesisitiza kuwa mazungumzo ndiyo njia bora ya kutatua tofauti zilizopo kati ya wauguzi na waajiri wao katika serikali za kaunti,akisema pande zote zinapaswa kuweka maslahi ya wananchi mbele na kuhakikisha kuwa huduma za afya zinarudi katika hali ya kawaida  

Amesema mgomo huo umeendelea kuathiri utoaji wa huduma katika hospitali na vituo vya afya vya umma katika maeneo mbalimbali nchini, huku wagonjwa wakikumbwa na changamoto katika kupata matibabu,wauguzi   wakishinikiza kutekelezwa kwa makubaliano mbalimbali ya ajira na kuboreshwa kwa maslahi yao ya kikazi, huku serikali za kaunti zikikabiliwa na changamoto katika kutimiza baadhi ya madai hayo.

Haya yanajiri wakati ambapo  katibu wa muungano wa wauguzi nchini Seth Panyako ameapa kwamba wahudumu wa afya hawatarejea kazini hadi pale ambapo serikali itatimiza matakwa yao chini ya mkataba wa makubaliano CBA

APERIT FM,HII NI YETU