You are currently viewing IDARA YA HALI YA ANGA YATOA TAARIFA NCHINI

IDARA YA HALI YA ANGA YATOA TAARIFA NCHINI

Maeneo kadhaa nchini yanatarajiwa kukumbwa na hali ya hewa kavu kuanzia leo Agosti 18, hadi Agosti 24 mwaka huu.

Kulingana na idara ya utabiri wa hali ya anga nchini, baadhi ya kaunti zinatarajiwa kupata mvua zikiwamo Bungoma, Trans Nzoia, Nakuru, Uasin Gishu, Kisii, Lamu, Kericho, Nyandarua na Nyeri.

Idara hiyo pia imetabiri vipindi vya baridi na mawingu katika kaunti za Embu, Kiambu, Kirinyaga, Laikipia, Meru, Murang’a, kaunti ya Nairobi, Machakos, Kajiado na Marsabit.

Pia imeonya kuhusu uwezekano mkubwa wa mvua za el-nino, uku ikitabiriwa kuwa mvua hizo zitaendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2027.

Kaunti ya Narok imetajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayoweza kukumbwa na maafuriko na maporomoko ya ardhi, hasa Narok mjini, Mosiro, Ewasing’iro, Kilgoris pamoja na maeneo mengine.

Idara hiyo inatarajia mvua kuwa chini ya wastani katika maeneo mengi ya Magharibi ya Kenya, kati ya Agosti na Oktoba mwaka huu kabla ya hali kubadilika, na mvua zaidi ya wastani kunyesha katika maeneo mengi kuanzia Oktoba hadi Novemba mwaka huu.

                                                                                                             APERIT FM, HII NI YETU