You are currently viewing Seneta Margaret Kamar Aunga Mkono Mswada wa Mfumo wa Anwani za Kitaifa

Seneta Margaret Kamar Aunga Mkono Mswada wa Mfumo wa Anwani za Kitaifa

Seneta wa Uasin Gishu Profesa Margaret Kamar ameunga mkono Mswada wa Mfumo wa Kutaja Barabara na Anwani za Mali, akisema si Wakenya wote wanaotumia au wanaoweza kufikia huduma za Google Maps.

Akichangia mjadala kuhusu mswada huo, Seneta Kamar alisema hatua hiyo ni mwanzo wa kuandaa na kupanga nchi kwa njia bora, hususan katika utaratibu wa kutaja na kutambua barabara.

Ameeleza kuwa mswada huo unalenga kuanzisha na kusimamia mfumo wa kitaifa wa anwani utakaorahisisha upatikanaji wa maeneo mbalimbali. Kwa mujibu wake, mfumo huo utasaidia huduma za dharura kama vile ambulansi kufika kwa haraka katika maeneo yanayohitajika, kwa kuwa wahudumu wataweza kutambua anwani sahihi bila ugumu.

Mswada huo unatarajiwa kuboresha utoaji wa huduma za umma, kurahisisha urambazaji wa maeneo, na kuimarisha mifumo ya dharura nchini.