Mwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Baringo, Florence Jematiah, ameonya dhidi ya mipango ya kuondoa masharti ya kiwango cha elimu kwa wanaotaka kuwania nyadhifa za kisiasa, akisema hatua hiyo inaweza kudhoofisha umuhimu wa kusoma na kuandika katika uongozi.
Kwenye kikao cha bunge Jematiah amesema kuondolewa kwa masharti hayo kunaweza kuathiri uwezo wa viongozi kutekeleza majukumu yao ipasavyo, hususan katika kuandaa na kutekeleza sera zinazolenga kuimarisha maendeleo katika ngazi ya kaunti na taifa.
Amesisitiza kuwa elimu ina nafasi muhimu katika kuwawezesha viongozi kuelewa masuala ya sera, kufanya maamuzi sahihi na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
APERIT FM,HII NI YETU

