Mbunge wa Keiyo Kaskazini Adams Kipsanai, ameiomba Kamati ya Bunge ya Elimu kutoa taarifa kuhusu utaratibu wa kuwasajili wanafunzi kutoka maeneo ya karibu katika vyuo na vituo vya mafunzo vya (KMTC).
Kipsanai anataka Kamati hiyo kufafanua vigezo vinavyotumika katika udahili wa wanafunzi wa maeneo yanayozunguka kampasi na vituo hivyo, pamoja na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha vijana wa eneo husika wanapata fursa za mafunzo ya afya.
Mbunge huyo pia anataka maelezo kuhusu sera na miongozo inayosimamia mgao wa nafasi za udahili, ili kuwe na uwazi na usawa kwa waombaji wote.

