Wakazi wa Kapchemutwa, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, wamepinga shughuli za ukataji wa miti kiholela ndani ya misitu, wakieleza wasiwasi kuhusu athari zake kwa mazingira.
Kulingana na wakaazi hao, iwapo shughuli hiyo itaendelea, itachangia kuharibu vyanzo vya maji na kusababisha athari kama vile kiangazi na mabadiliko ya tabianchi.
Wameitaka KFS kuandaa kikao maalum cha mashauriano kuhusu mchakato wa uvunaji wa mbao, huku wakisema hawatakubali tenda yoyote inayolenga kusababisha madhara kwa mazingira.
Haya yanajiri wakati ambapo Shirika la Huduma za Misitu nchini, KFS, limekanusha madai ya ukiukaji wa sheria na kutetea shughuli hizo, likisema zinafanyika kwa mujibu wa taratibu na sheria zinazosimamia usimamizi wa misitu.
APERIT FM,HII NI YETU

