Naibu Rais wa Kenya, Prof. Kithure Kindiki, amesema maandalizi ya uzinduzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Lamu yamekamilika, huku uzinduzi rasmi ukipangwa kufanyika Septemba 30.
Kwa mujibu wa Kindiki, mradi huo ni sehemu ya mipango ya serikali ya kuimarisha sekta ya mafuta na nishati nchini pamoja na kuongeza shughuli za kiuchumi.
Amesema kiwanda hicho kinatarajiwa pia kuwa na mchango katika kuimarisha thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya dola ya Marekani, huku kikitoa fursa za ajira kwa mamia ya vijana nchini.
Kindiki amesema serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha miradi ya nishati inachangia ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
APERIT FM,HII NI YETU

