Mbunge wa Kacheliba, Titus Lotee, ametoa wito kwa serikali kuendesha zoezi la kina la kutwaa silaha haramu katika maeneo ya rumos na morita,akisema ndo chanzo cha matatizo ya ukosefu wa usalama eneo hilo
Lotee pia ameitaka serikali kuwatuma maafisa wa KPR , katika maeneo hayo ili kushirikiana na wale wa KDF kuimarisha usalama na kulinda maisha na mali ya wananchi.
Ameonya kuwa kushindwa kuchukua hatua za haraka kunaweza kuwalazimu baadhi ya wakazi kuanza kuchukua sheria mikononi , akiweka bayana haja ya usawa katika mchakato wa kutwaa silaha haramu mikononi mwa raia ili kurejesha usalama
APERIT FM,HII NI YETU

