You are currently viewing WITO WA AMANI BONDE LA KERIO

WITO WA AMANI BONDE LA KERIO

Wito umetolewa kwa jamii za eneo la Bonde la Kerio kudumisha Amani na umoja na kujitenga na visa ambavyo vinasababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Akizungumza katika hafla ya kubuniwa Chama Cha Amani katika Chuo cha mafunzo ya walimu cha Chester eneo bunge la Sigor Kaunti ya Pokot Magharibi, mshirikishi wa tume ya Uwiano na Utangamano wa kitaifa NCIC eneo la Kaskazini mwa Bonde la Ufa Victor Kabulemi, amesema jamii hizi zitaweza tu kuhusika katika ujenzi wa taifa iwapo kutakuwa na mazingira tulivu.

Pia, kulingana na Afisa wa Mipango katika Kanisa la Free Pentecostal Fellowship in Kenya (FPFK) Alex Eregei, kubuniwa kwa chama cha amani kwenye chuo hicho kutasaidia pakubwa katika kubadili mtazamo wa uhusiano ambao umekuwepo kwa miaka mingi baina ya jamii za eneo hilo.

Hata hivyo uongozi wa chuo hicho ukiongozwa na mwalimu mkuu Jonathan Kiprotich umeelezea umuhimu wa chama hicho cha amani katika kuwasaidia wanafunzi kujieleza kwa uwazi, ukitoa wito kwa wadau mbalimbali wa amani kuwaunga mkono katika safari hii ya kuhakikisha amani miongoni mwa jamii na taifa kwa ujumla.