Naibu Rais Kithure Kindiki amesema kuwa kutojiamini ni moja ya viungo muhimu vinavyokosekana katika juhudi za Kenya na Afrika kufikia maendeleo na ustawi wa kiuchumi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya muda mrefu nchini, kindiki amesema Bara la Afrika lina rasilimali nyingi, ardhi yenye rotuba na idadi kubwa ya vijana, lakini bado linahitaji kujenga imani katika uwezo wake wa kufanikisha maendeleo.
Amesisitiza kuwa kenya inapaswa kulinda dira yake ya maendeleo ya muda mrefu kupitia mifumo thabiti ya kisheria ili kuhakikisha mipango ya maendeleo inaendelea bila kuathiriwa na mabadiliko ya kisiasa. Naibu Rais ameongeza kuwa sekta za kilimo, madini, viwanda, elimu, sayansi, teknolojia na ubunifu ni nguzo muhimu za kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi

