Kenya imepata heshima kubwa ya kuandaa mashindano ya dunia ya riadha mwaka wa 2029, baada ya taifa hilo kushinda zabuni dhidi ya Miji ya London nchini Uingereza, Rome nchini Italia na Munich nchini Ujerumani.
Uamuzi huo umetangazwa na shirikisho la riadha duniani baada ya kikao cha baraza lake mjini Budapest, Hungary.ushindi huo unaifanya Nairobi kuwa mji wa kwanza Barani Afrika kuandaa mashindano ya dunia ya riadha, hatua inayochukuliwa kuwa ya kihistoria kwa kenya na bara la afrika kwa ujumla.
Rais wa shirikisho hilo Sebastian Coe, amesema Nairobi iliwasilisha zabuni yenye mvuto mkubwa, huku akitambua uhusiano wa muda mrefu kati ya kenya na mchezo wa riadha.
Amesema kenya tayari ina historia ya kuandaa mashindano makubwa ya riadha, ikiwemo mashindano ya dunia ya vijana chini ya miaka 18 mwaka 2017 na mashindano ya dunia ya vijana chini ya miaka 20 mwaka 2021.
Mashindano ya mwaka 2029 yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Kasarani, ambao unaendelea kufanyiwa ukarabati. Hatua hii sasa inaweka Nairobi katika ramani ya dunia kama kituo muhimu cha mashindano makubwa ya riadha.
APERIT FM ,HII NI YETU

