Chama cha kitaifa cha walimu, kuppet, kimeitaka tume ya huduma za walimu, TSC, kuongeza idadi ya walimu wanaopandishwa vyeo, ili kuwapa walimu motisha na kuboresha utoaji wa elimu nchini.
Kuppet imesema idadi ya walimu wanaonufaika na nafasi za kupandishwa vyeo bado ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya walimu wanaostahili kupanda katika viwango vya juu vya taaluma.
Kuppet sasa inaitaka tsc kuongeza nafasi za kupandisha vyeo na kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa uwazi, haki na kwa kuzingatia sifa, uzoefu pamoja na utendakazi wa walimu.
Chama hicho pia kimeitaka serikali kutenga fedha zaidi kwa ajili ya ajira na maendeleo ya walimu, ikisema idadi kubwa ya wanafunzi pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya elimu kunahitaji kuwa na walimu wa kutosha katika shule za umma.
Kuppet imesisitiza kuwa kupandishwa vyeo kwa walimu si suala la maslahi yao pekee, bali ni hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya elimu, kuongeza motisha kazini na kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora ya elimu.

